BASIC NEED
Deo Moshi
August 27, 2026
2 min read
165 views
1 favorites
Open Access
Umuhimu wa hitaji la upendo kwenye jamii na dunia yetu
BASIC NEED
Mtaala mpya wa elimu uletwe ukiwa na basic need nne sio tatu tena..
...Badala tu ya malazi, mavazi na makazi iongezwe na Mapenzi!
Kuna masomo hautafundishwa kwa kukosa makazi
Zipo topic hautazielewa sababu ya kukosekana malazi wala mavazi..
Ndio!
Mitihani ya upweke hainaga majibu ya kuchagua, ina jibu moja tu la kukosa mapenzi.
Watu wanauana, wanajiua kwasababu ya wivu wa mapenzi sio wivu wa maendeleo.
Familia zinatengana sio kwa kutokuwepo kwa malazi, makazi au mavazi..
...Sababu kubwa ni ileile ya kutokuwepo kwa mapenzi kati yao
Sijawahi kuona mtu aliyeumizwa na mapenzi akiponywa na familia yake.
Lakini nishawahi kuona mapenzi yakimponya mtu aliyeumizwa na familia yake
Ieleweke mapenzi nnayoandika hapa sio yale ya mtu na mpenziwe tu.
Ni mapenzi kiujumla anayohitaji kupatiwa mimi, huyu, yule na wewe unayesoma hapa.
Kuna usalama dunia inakosa kutokana na ukosefu wa kukosekana kwake
Ulimwengu umekua sehemu ya hatari kuishi kwaajili ya watu hawana mapenzi kati yao.
Watoto wa mitaani, ukatili wa kila aina unaofanyika duniani chanzo kikuu ni hiko.
Binadamu wamekua wanyama kisha wanyama ndo wamekuwa na ubinadamu siku hizi.
Watu wanaishi kwa kunafkiana badala ya kupendana.
Ndugu, marafiki, wanandoa wote hao migogoro mingi inaanzia kwasababu hakuna mapenzi baina yao.
Urithi pekee ambao koo imekua nadra kuachiana, zikagawanyika na kutengeneza matabaka.
Vizazi kwa vizazi vikaishi na kuishia ndani ya mgawanyiko huo ulioletwa kwa kutokuwepo kwa mapenzi katika kizazi chao.
Tumefikaje hapa? Na nani wa kututoa tulipo tunapoelekea ni pabaya mno..panatisha.
Najua vizuri sana kuhusu chuki, huwa inakuwa na sababu ya uwepo wake
Ni upendo pekee ndio unaweza ukawepo bila sababu
Mpe mtu yeyote makazi mazuri, malazi yanayovutia na mavazi yanayompendeza.
Halafu mnyime mapenzi tu, ni rahisi sana kwake kuona vyote ulivyompa si chochote.
Bado tu hamjaelewa kwanini mapenzi ndio basic need muhimu zaidi kwa jamii?
Ningekua Rais au Waziri wa Elimu ningeyaweka kwenye MTAALA!